ZIFAHAMU TABIA ZA WAJASIRIA MALI WANAOFANIKIWA
Mjasiria
Mali ni nani
Ni mwanzilishi mmbunifu mtu mwenye wazo na mtekeleaji wa
mawazo ya kibiashara,ni mtu ambaye anauwezo wa kuona fursa nakuamua kuzifanyia
kazi zile fursa kwa ajili ya manufaa chanya iwe katika sekta ya
kilimo,usafiri,uuzaji bidhaa au
utaalamu na kuweza kutengeneza faida kupitia shughuli hiyo
1. Kuona fursa/Maono/Mawazo(Visualization)
Mjasiria mali yeyote hua na
uwezo wa kuona fursa kabla hata ya watu wengine kuweza kuziona na ni watu walio
namaono ya mbali na kujua vitu gani vitahitajika baada ya mda Fulani hivyo wao
mawazo yao hufurika fursa mbalimbali na kuchagua kitu kipi wakifanye na
kukigeuza kua fedha.
2.Hufurahia kufanya vitu wavipendavyo
Wajasiria mali vyema na watewengi hupenda kufaya vitu
viwapavyo furaha na ndio maanda hufanikiwa kwani katika kufanya kazi kwao hua
ni njia mojawapo ya kufurahia maisha hivyo hua na mawazo ya kibiashara
yawafurahishayo na ambayo hupokelewa vyema na wateja wao.
3.Wanauthubutu
Wajasiria mali na
watu walio na uthubutu ambao hupambana na uoga wao na kufanya vitu wavitakavyo
hiyo huhusisha kupoteza fedha katika mawazo wayaaminiyo na pia huhusisha uwezo
wao wa kuamua na kuaznisha kitukatika mazingira hata yasiyo rafiki na hata kwa
mitaji midogo.
4.Wanafanya kazi kwa bidii
Wajasiria mali wanaofanikiwa hua
na tabia ya kufanya kazi kwa bidii kama ni kutoa huduma kama ni kuuza bidhaa
huhakikisha mteja hasikitiki kwa sababu ya wao kushindwa kukamilisha kazi au kata
huduma kwa mda.
5.Ubunifu
Wajasiria mali wanaofanikiwa
siku zote hua wabunifu na watu wa kujifunza vitu vipya ili kuweza kutoa huduma
bora au bidhaa bora na siku zote kujiweka katika chaguo bora katika jamii
wanayofanya kazi.
6.Kupambana na uoga/hawaogopi kujaribu
Wajasiria mali na watu wanaoamua
kuushinda uoga ,kutojari kukataliwa ila huogopa kupoteza nafasi kwa
kutokujaribu kabisa pia ni wapambanaji katika mawazo wanayoyaamini na
kuyafanyia kazi kwa kupambana na vikwazo vyovyote vinavyoweza kujitokeza.
7.Hawajari Mitazamo/Hawaogopi kua tofauti
Wjasiriamali wanaofanikiwa
hutengeneza dunia yao wenyewe ambapo huishi kwa kufuata taratibu zao na sio
mitazamo ya watu wengine wanavyotaka waishi mfano mjasiria mali anaweza kua
kamaliza chuo ambapo inategemewa anatakiwa kuvaa tai au suti na kuonekana
akienda kufanya kazi sehemu Fulani wao huweza kuamua kuvaa buti na kwenda
shamba ilimradi anajua manufaa yake baada ya mda Fulani ambayo huweza kua
makubwa kuliko yule anayeonekana bora akienda kufanya kazi kwa mtu.
8.Ni watendaji si wafikiriaji tu
Wajasiriamali wanaofanikiwa hawa
ni watu ambao wazo ikiwajia na wakilichanganua na kuona manufaa yake huamka na
kwenda kulifanyia kazi si kuendelea kufikiria sana jinsi gani wazo
litashindikana hawa ni watendeaji wa mawazo.
9.Wanajiamini.
Wajasiriaa mali wanaofanikiwa ni
watu wanojiamini kwani siku zote wao hua watu wa tofauti katika jamii na
hufikiri vitu ambavyo jamii huona haviwezekani hivyo husimamia mawazo yao na
hata mwisho kuweza kuthibitisha mawazo yao kwa jamii nayo kuweza kuwaamini kua
inawezekana.
10.Wanamawazo chanya
Wajasiriamali wanaofanikiwa
hutawaliwa na mawazo chanya Zaidi na sio hasi na hiyo ndio siraha kubwa walio
nayo kwani huchambua mambo kabla ya kuyafanya na kwa sababu wao huchukua
risk/kujaribu hiyo huwafanya wao wawaze chanya ili kufikia malengo yao kwani
mtu mwenye mawazo hasi hawezi kupiga hatua yoyote kwani anauhakika wa kushindwa
tayari.
11.Wavumilivu.
Wajasiria mali
wanofanikiwa ni watu wenye uvumilivu wa hali ya juu ukiangalia mianzo ya
bishara mbalimbali ni ya kukatisha tamma na ni wachache ambao huamini kufika
kwake ila wao hupambana wakitegemea mema na hiyo ndio huwafanya wao pekee
kusimama ingali wengine hushia njiani na biahsara zao kufa.
12.Wanatabiaa za uongozi/waanzilishi.
Wajasiriamali wanofanikiwa wana
tabia za uongozi ambazo ni kua na maono/vision pia utendaji wa vitendo kuhakikisha
kufikia ile vision sio watu waelekezaji ni waelekezaji watendaji wanaotangulia
mbele hivyo wao huwa na uwezo wa kujua vitu wanavyotaka vifanyike na huwa
wataalamu mara nyingi kuliko wanaoongozwa kwani wao ndio wenye mawazo na
hupokea mawazo/au ushauri na kujifunza.
13.Wanaadabu/Kuheshimu fedha
Wajasiriamali wanaofanilkiwa hua
na heshima kubwa ya kila wanachopata kama fedha si watu wafujaji wa hovyo wa
fedha hiyo huwasaidia kupata nafasi ya kusonga mbele na kuweza kupanua na
kukuaza biashara zao.
14. Wananjaa ya kutimiza malengo
Wajasiriamali wanofanikiwa
wananjaa kubwa ya kutimiza malengo yao si watu ambao wanataka kitu Fulani na
kukiacha wakiamua jambo hulisimamia mpaka kufanikiwa kwake.
15.Hawatabiriki
Wajasiria mali ni watu usioweza
kuwatabiri wanafikiri nini katika wakati huu kwani vichwa vyao mda wote hua
vinakua katika kufikiria tu na kubuni vitu vipya unaweza kunakili wazo hili na
wakaibua wazo jipya hivyo mawazo yao ni mawazo endelevu.
16.Hawaishi kwa maonyesho wanajali kazi zao
Wajasiriamali wanaofanikiwa wo
huishi maisha ya kipekee hawafanyi maigizo katika maisha labda kufanya maigizo
ni moja ya matangazo ya biashaa yao ila huamua kufanya vitu vilivyo na faida
kwao.
18.Kujenga uamninifu
Huamua kujenga uaminifu katika
jamii inayowazunguka au watu wanaofanya nao biashara ili kutengeneza mazingira
yao ya kudumu katika bishara.
Zilizoorodheshwa ni baadhi ya tabia muhimu kiutafiti ambazo zinapatikana kwa wajasiria mali wengi waliofanikiwa.
Imeandikwa na by:Stanley
Mkolangunzi
Blogger:biznessstartupsecrets.blogspot.com
Hi,
ReplyDeleteInteresting article! Thank you for sharing them! if you want Top 10 auditors in bangalore Top 10 audit fims in bangalore click on it