Faida za kuanza na mtaji mdogo katika biashara
Faida za kuanza na mtaji mdogo katika biashara
Watu
wengi ni wajasiriamali wanaotamani
kuanza bishara nao wana mawazo mazuri ya kuweza kuanzisha biashara ila
hujikuta wamekwama kwa tatitzo la kukosa mitaji kwa ajili ya kuanzisha biashara
au kuyafanyia kazi mawazo yao walionayo wanayoamini yanaweza kuwatoa toka
sehemu moja kiuchumi hadi sehemu nyingine.Lakini katika msisitizo wangu kwa
wote mnaosoma Makala zangu usiogope kwa kua na mtaji mdogo na kutaka mpaka uwe
na mtaji mkubwa ili uanze kufanya biashaara ila anza tu .na Kama mtaji unao
mdogo kabisa lakini unakuwezesha kuanza usisubiri kumiliki mamilioni ili kuanza
kutendea wazo lako .
Faida za kuanzisha
biashara ukiwa na mtaji mdogo
1.Unapata nafasi ya kuwajua wateja
wako.
Kwa kuanza na mtaji mdogo unapata
nafasi ya kuwajua wapi ni wateja wako unajua umri wao,kipato chao ,tabia
zao,tamaduni zao hivyo huo ni utafiti ambao unaufanya kwa kutumia mtaji mdogo
huku unatengeneza faida yako kupitia biashara ndogo.
2.Unajifunza jinsi ya kutumia vyema
rasilimali ulizonazo
Unajifunza matumizi bora ya
rasilimali ulizonazo kwani katika kipindi hicho ukiwa umeamua na unania ya kua
mjasiriamali mkubwa utajitahidi kutumia mbinu mbalimbali za kuhakikisha wateja
wako wanafurahi utajifunza mbinu mbalimbali za kupata bidhaa na mbinu
mbalimbali za kuhakikisha rasilimali ndogo zinatoa huduma bora kwa wateja mfano
unatoa hela kidogo kwa supplier wako na kumwomba aje achukue baada ya mda ili
ukiuza ile fedha yake umlipe hivyo unatengeneza faida yako na supplier unamlipa
na mteja wako kafurahi lakini kwa robo ya mtaji uliohitaji kua nao kufanya
biashara hiyo
3.Unapata nafasi ya kukuza ndoto yako
na kufikiri Zaidi
Mtaji mdogo unapata nafasi ya
kufikiri zaidi ni vitu gani unatakiwa viboresha lakini pia unapata fursa ya
kuona mambo mbalimbali unayoweza yapanua ukipata mtaji na ndoto ya kipindi upo
katika utendaji itakuwezesha wewe kuwa na mawazo mapana yaliyo kiutendaji na
yenye asilimia kubwa ya mafanikio.
4.Unapata wateja utakao kua nao katika
biashara
Katika kipindi hiki unapata nafasi
ya kua na wateja ambao watasimulia mwanzo wako ambao huweza kua nawe na kua
mabalozi wa biashara yako jinsi inavyokua jinsi siku zinavokwenda.
5.Unajua nini wateja wako wanahitaji .
Kipindi unabiahsara yako ukiwa na
mtaji wako wateja wako katika eneo uliloamua kufanya biashara watakuja na
maswali kuulizia huduma wanazozihitaji ni wewe kutumia maswali yao na kujua ni
vitu gani unapaswa viongeza ukipata mtaji ili kukuza biashara yako.
6.Inakuepusha kupata hasara
Inakuepusha kupata hasara isiyo ya msingi
mfano wakati naanza biashara yangu niliweka blueband katika mtaa uliokua mpya
na wateja wengi walikua ni wenyeji wasio na mazoea ya matumizi ya blueband
hivyo niliweka boxi kadhaa ila kilichotokea bidhaa ile ilikaa mpaka iliexpire
.kosa moja nilifanya research lakini haikujitosheleza lakini kwa bahati sababu
nlikua na mtaji mdogo baadhi ya vitu nlivoshindwa kufanya wateja waliviitaji
nlipopata fedha nkaviweka mwitikio wake ulikua mzuri sikuwahi kuweka bidhaa
iliyoniharibikia nikapata hasara tena.
7.Unapata nafasi ya kuunda brand
yako/Unajitangaza
Kipindi ukiwa na mtaji mdogo unapata
nafasi ya kujitangaza waweza kutambulisha kijiwe au unaanza kujulikana kidogo
na taarifa husambaa sana hivyo kipindi umepata mtaji unakua umekwisha fahamika.
Hivyo ni vizuri kama umeajiriwa na unategemea baada ya mda fulani utataka
ujiajiri anza kujitambulisha hivyo hata kama una mtaji mdogo anza itakua na
faida kubwa kwako hapo mbeleni.
8.Biahashara ya mtaji mdogo ni chambo
Ukiwa na biashara hata kama ina
mtaji mdogo na hujui utapata vii mtaji basi ile biashara yako ni chambo cha
kukupatia mtaji mkubwa .mfano nilianza nikiwa na biashara ndogo kabisa lakini
kwa bahati nzuri kuna benki waliita wakasema kama utahitaji mtaji tunaweza
kukupa uongezee ili kubororesha biashara yako lakini hakuna atakayekuongezea
kama hujaanza kutafuta.
Lengo kuu la
Makala hii ni kukuambia kwamba usijali unakidogo kiasi gani anza kupitia hicho
ulicho nacho na hatua ya kwanza utakayopiga itazalisha hatua ya pili ila ukikaa
na kusubiri huwezi kuanza wala fika popote katika mapambano ya mafanikio au
hasara unayoweza pata utapata mtaji wazo lako la biashara likiwa limekwisha mda
wake sipendi useme ningejua ningeanza na fedha ile ndogo wakati unamuona
aliyeanza na fedha kidogo .Musa aliulizwa umeshika nini mkononi wewe umeshika
nini mkononi hivyo ulicho nacho kinatosha kukuvusha katika bahari ya umaskini
au kukufanya ufurahie maisha yako kwa kutimiza ndoto zako .kama unataka kua
consultant,engineer mwimbaji mchekeshaji,mwigizaji anzia hapo ulipo.
Imeandaliwa na
Stanley Mkolangunzi
Entrepreneur &Motivational speaker
Blog:biznesstartup secrets
.blogspot.com
Youtube:Skills& Motivations TV
Nawashukuru sana, leo naanza kwa kufuata ushauri wenu, nitaendelea kuwafuatilia na nitawapa muelekeo wa biashara yangu.
ReplyDeleteKaribu tena tujifunze inawezekana kuishi ndoto yako mjuze na mwingine apae maarifa kupitia blog yetu
DeleteHi,
ReplyDeleteI having many kinds of knowledge from your blog.. keep sharing !if you want tax return services bangalore list of audit firms bangalore click on it