Jinsi ya Kuongeza Mauzo kwa kuzingatia Fikra za mteja

 

JINSI YA KUONGEZA MAUZO KWA KUZINGATIA FIKRA ZA MTEJA

Katika vitu nimejifunza katika biashara na baada ya kufanya utafiti juu ya wateja wengi ni kwamba mteja anapokuja katika biashara yako si kwamba anakuja kwa sababu sehemu nyingine hakuna bidhaa kama hiyo ila ni kwamba kwako anapata bidhaa Zaidi ya hivyo vitu anaweza pata sehemu nyingine.

Unapofanya biashara ukiweza kujumuisha na hisia unaweza washawishi wateja wengi Zaidi kwani hisia humfanya mtu kua mtumwa wake na hivyo kuna fursa ya kuongeza mauzo na mapato kama utaweKa na bonus ya hisia katika bidhaa au huduma zako.

1.Mteja wa thamani

Kuna huduma zinaitwa mteja wa thamani hii ni huduma wengi tumekutana nayo mfano katika mabenki au katika huduma mbalimbali watu hua tayari kutoa fedha zao ilimradi kwanza wapewe kipaumbele cha thamani hata kwa kuongezewa vitu vidogo sana lakini wapo tayari kutoa fedha Zaidi kwa sababu wameitwa na wameonekana wa thamani.

2.Hisia ya kwamba ni bei rahisi

Hiyo ni hisia ambayo mteja anatengenezewa kwamba kununua katika utaratibu Fulani itamfanya alipe kwa gharama ndogo Zaidi mfano ukilipa kifurushi cha mwaka unapata punguzo la 20% na ukilipa kila mwezi itakua gharama 100% hivyo mteja akipata hiyo fikra na hisia anaweza kua tayari kulipa kwa mwaka au jumla  ili tu apate huo upendeleo wa punguzo la bei.

3.Hisia kwamba yeye ndio wa kwanza na amepewa tofauti

Mashirika mbalimbali wanatumia njia tofauti kuhakikisha kua wanatengeneza mfumo ambao utawawezesha wateja kupata huduma ambayo itategemea matakwa ya mtu na mapenzi ya mtu sio bidhaa ambayo kila mtu anayo.mfano kama unataka suti unashonewa kwa kufata vipimo vyako na kama kuna kitu unataka kiongezeke unawekewa.na wamekua wakitumia taarifa hivyo mteja anapofika wanachukua taarifa zako lakini pia kwa kutumia teknolojia wanaweza kufatilia taarifa zako na kufanya utafiti juu yako kwa mifumo inaitwa analytics kujua vitu unavyopenda,tabia na matumizi yako na wafanyabiashara wengi wadogo kwa wakubwa wamekua wakifanya hivyo mfano kuna mtu alikua anauza mitumba akachukua namba ya dada Fulani kila akifungua mitumba mipya alimpigia simu  yule dada na kumwambia nimefungua kabla sijawaita watu wengine njoo uangalie wewe kwanza na huyo dada alikua akienda lazima anunue .

4.Hisia za uharaka katika upatikanaji wa huduma au bidhaa na urahisi wa upatikanaji bidhaa

Mfanya biashara akiweza kumpa mteja hisia kwamba akienda kwake atapata huduma haraka na kwa urahisi bila usumbufu ana uwezo wa kuvutia wateja wengi Zaidi.mfano kumekua na vilinganishi mbalimbali vinatumika kuangalia ni nchi gani unaweza kwenda kufungua kampuni kwa urahisi katika Africa kuliko nchi nyingine na wapi ni gharama rahisi hivyo mfanya biashara akiweza kutengeneza hisia hiyo pia na kuweka mifumo inayomfanya huduma zake zipatikane kwa urahisi anaweza pata wateja Zaidi mfano biashara kwa mtandao nk.

 Imeandaliwa na :Stanley Mkolangunzi

Comments


  1. Very Informative and creative contents. This concept is a good way to enhance the knowledge. thanks for sharing.
    Continue to share your knowledge through articles like these, and keep posting more blogs.
    And more Information Enterprise application for Construction

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Faida za kuanza na mtaji mdogo katika biashara

S&T HANDCRAFTED FASHIONS AND TOURISM

ZIFAHAMU TABIA ZA WAJASIRIA MALI WANAOFANIKIWA