ZIFAHAMU FAIDA ZA KUA MJASIRIA MALI
Ni mwanzilishi mmbunifu mtu mwenye wazo na mtekeleaji wa
mawazo ya kibiashara,ni mtu ambaye anauwezo wa kuona fursa nakuamua kuzifanyia
kazi zile fursa kwa ajili ya manufaa chanya iwe katika sekta ya kilimo,usafiri,uuzaji bidhaa au utaalamu na kuweza kutengeneza
faida kupitia shughuli hiyo
1. Unakua kiongozi wa maisha yako
Unaapokua mjasiria mali unapata nafasi ya kua na maamuzi
ya maisha yako na wapi unataka kwenda na wapi au kwa kiasi gani unaeza fikia
kwa malengo yako ya kimaisha kwani ukiajiriwa utakua ukishi kwa mnyororo
ulopangiwa na mjasiria mali aliyeanzisha
hiyo kampuni unayoifanya kazi.
2.
Uhuru
Mjasiria mali anapata uhuru wa kufanya mambo yake na
kupanga ratiba zake pia kuweza kufurahia maisha si kama muajiriwa ambaye mda
wake unaendeshwa na mwajiri wake inakupa nafasi ya kushiriki mambo yako ya
kijamii unapata nafasi ya kujaribu mambo mbalimbali katika maisha.
3.
Kipato kisicho na kikomo
Unaeza
kujitengenezea kipato kisicho kikomo ni vile utavokua biashsara yako
ikiongezeka ndivyo kipato kitavyoongezeka ambacho utakua na mamlaka ya kiasi
gani unataka kujilipa
4.Uchaguzi
wapi uishi
Unapokua mjasiria mali unakua na muamuzi mmoja aliye
rafiki yako ambaye ni mteja hivyo unauamuzi wa kuishi popote pale wateja wako
walipo si vile kupelekwa sehemu mida mingine hupendi kua katika maeneo yale .
5.Uwezo
wa kuzitumia fursa
Unapokua mjasiria mali unapata nafasi ya kuweza kuzipata
fursa kwa urahisi Zaidi ukilinganisha na ukiwa mwajiriwa ambaye mda wako
unaendeshwa na vigumu kwenda kutumia fursa zinazopatikana katika mazingira na
jamii.
6.Unakua
wewe ndio Boss/nafasi ya kua mmiliki
Unapokua mjasiria mali wewe ndiwe uliye na maamuzi juu
yako na mshauri wako nimteja wako ambaye siku zote wapaswa muheshimu kwani
ndiye anayekufanya uwe boss.
7.Nafasi
ya kufanya kazi itayoishi vizazi
Ukiwa mjasiria mali unaeza anzisha biashara au shughuli
ambayo vizazi vitaweza kufaidi kupitia wewe na kukumbuka kwa kuwasaidia ,kutoa
ajira na misaada kwani ukiwa mmiliki ni rahisi kukumbukwa kuliko ukiwa
mfanyakazi ambaye anabadilishwa kwa vipindi tofauti kutegemeana na kampuni au
shirika linavyoenda.
8.Kutengeneza
ajira kwa watu
Unapokua mjasiria mali unatengeneza ajira kwa watu
wengine hivyo kwako inakupa nafasi ya kusaidia maisha ya watu wengine walio
katika hali ngumu.
9.Unafanya
kile kitu unakipendenda
Unapokua mjasiria mali unapata nafasi ya kufanya shughuli
unazofurahia kuzifanya katika maisha yako na pia unapata nafasi ya kua mfano wa
kuwavutia wengine katika maisha kuanza kufanya vitu wavipendavyo.
10.Unapata
nafasi ya kubadili dunia
Njia pekee ya kuweza kufanya mabadiliko ya kitu Fulani ni
wewe kusimama na kuanza kufanya kitu chako kitakachokua na manufaa katika jamii yako yale uyapendayo
hivyo unauwezo wa kusogeza huduma Fulani sehemu na kufanya maisha ya jamii ile
kuboreka na kuleta mapinduzi chanya.
Faida
nyingine
Unapata nafasi ya kuishi ndoto zako unapata nafasi ya
kuijaribu Imani yako unapata nafasi ya kufurahia kupitia mambo uyaaminio na
kufurahia masiha katika namna ya kipekee na watu au timu yako utayoiunda.
Hizi ni sababu zangu kumi kwa nini uwe
mjasiria mali katika maisha yako naamini nimeamsha hulka na kukupa maana kwa
nini uwe mjasiria mali.
Stanley Mkolangunzi-Blogger:Biznessstartupsecrets.blogspot.com
Phone : +255 764-098564
Email : smkolangunzi@yahoo.com
Comments
Post a Comment