Madhara yatokanayo na mitandao ya kijamii
Madhara yatokanayo na mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ,ni mitandao inayotupa nafasi sisi binadamu kupashana habari na kupeana taarifa juu ya mambo yanayotokea sehemu nyingine katika dunia au sehemu ya mbali na ni njia mojawapo yakuwakutanisha watu waliopoteana kwa mda mrefu ili mradi waweza kukumbukana kwa majina au utambulisho wao na pia inatoa nafasi ya kuwasiliana na watu tusiofahamiana.mfano wa mitandao ya kijamii “Facebook,Intagram,Whatsap,Youtube,snapchat,twitter etc.
Mitandao ya kijamii inavyofanya kazi
Wametengeneza mfumo ambao umekua ukitumia saikolojia ya mwanadamu kumuendesha aweze kushinda katika mitandao hiyo ya kijamii na kwa mda mwingi wanye mitandao wamekua wakifatiliwa nini mtumiaji anafanya katika mitandao hiyo ya kijamii hivyo hiyo mitandao imekua ikitumia taarifa hizo kumfanya mtumiaji kurudi mara kwa mara akijirudia kila mda kwa kufatilia mapendekezo yanayotolewa tokana na tabia na vitu avipendavyo ambavyo kuna wakati vimekua vitu potoshi na si vya kumjenga mtu,lakini watu wamezidi kua watumwa wa mitandao hiyo ya kijamiI.
Madhara yatokanayo na mitandao ya kijamii
1.Kupoteza umakini
Mitandao imefanya watu kupoteza umakini mara nyingi kwa sasa mda mwingi umekua ukitumika kujadili mambo katika familia zetu kwa sababu tunahitaji tumia mda Zaidi kusisitiza jambo kwa sababu mtu anasikiliza huku akiwa facebook au watsap na Instagram.
2.Kuharibu mahusiano
Mitandao imeharibu ndoa mbalimbali katika maisha watu wamekua watiifu kujibu post toka kwenye mitandao kuliko kuhudumia familia zao au kuwajibu watu wao wa karibu vizuri lakini mtu yupo radhi atumie mda mrefu kufikiri namna ya kujibu katika mtandao kuliko ajibu vipi kw amtu wa karibu.
3.Kupoteza mda na hasara katika kazi na biashara
Kupoteza mda mwingi watu wamekua wakitumia mda mwingi katika mitandao ya kijamii kuliko mda unaotumika katika kutenda kazi zao hivyo kupoteza na kuleta hasara katika mashirika mbalimbali na biashara zao mfano mtu anauliza bei ya bidhaa mhudiaji anakujibu macho yakiwa whatsap au instagram bila kumuangalia mteja hivyo mteja huweza kuamua kwenda anakoona anathaminiwa.na pia mda mwingi mtu anatumia Zaidi ya masaa matatu akiangalia kinachoendelea katika mitandao ya jamii na mda mwingine katika kazi watu wamekua watumwa kwamba lazima ajibu awe active katika mitandao ya kijamii.
4.Chanzo cha migogoro na mporomoko wa maadili
Mitandao ya kijamii imekua chanzo cha migogoro katika jamii zetu mfano watu wamekua wakizusha mambo katika jamii yasiyo na uhalisia hivyo kufarakanisha watu mfano mtu anataka kuuza taarifa zake anatumia mitandao ya kijamii kuandika mambo yake ambayo mwisho wake watu kufarakana.Kuharibika kwa maadili mitandao ya kijamii imekua sababu kubwa ya kupoteza maadili watu wamekua wakiweka picha zao za utupu ili kupata umaarufu bila ya kujali watu wanatazama picha hizo mfano Tanzania imekua changamoto mfano wasanii wamekua wakiingia na kutekwa na mitandao ya kijamii kwa asilimia kubwa na kuona kua ni sawa ila cha msingi tunapaswa tukumbuke tamaduni zetu lakini tusisahau mambo tuyafanyao yana madhara katika vipindi vya mbele ndio maana kuna baadhi ya watu wameamua kufuta vitu walivyokua wakiweka katika mitandao hiyo ya kijamii kwa sababu leo yao inakinzana na mambo walokua wakiyapost bila kujua madhara yake.
5.Upotoshaji
Upotoshaji wa kijamii mfano kumekua na kesi katika nchi mfano marekani kwamba uchaguzi uliathiriwa na mitandao ya kijamii ambayo ilikua ikifanya kampeni zisizotakiwa fanyika hivyo kusababisha watu kupiga kura kwa watu labda walitakiwa wasipigiwe kura mpaka ikafikia kiongozi wa facebook kwenda kushtakiwa hivyo kuna upotoshaji wa namna nyingi katika mitandao ya kijamii.taarifa za uongo uzushi nakuharibiana wadhifu na mambo mengine ya kuharibu wadhifu wa mtu.
6.Uongo
Mitandao ya kijamii imekua njia ya watu kujificha na kudanganya kupotosha watu ukiangalia mitandao ya kijamii watu wamekua wakitumia picha a watu wengine au vitu vya watu wengine mfano magari nyumba au mavazi kumbe wameazima na hivyo kuwapotosha vijana kuwafikirisha wanafanya mambo Fulani au kuwavutia watu kufanya baadhi ya mambo kana kwamba mafanikio yake ni rahisi kumbe si kitu cha kweli kwamba ukweli kupata vitu hivyo ya pasa mtu kufanya kazi kwa bidii kujifunza sana kujua uvumilivu wa hali ya juu kufikia katika viwango hivyo lakini watu wamekua wakipata marafiki kwa kuangalia sura ambazo mda mwingine sio za kwao hivyo kuleta matatizo pale wanapokuja kuonana kutokana yaliyoonekana katika mitandao na uhalisia havifanani na baadhi ya watu wamewahi kupata matatizo ya kukutana na watu wa ajabu tokana na uongo uliomo katika mitandao ya kijamii.
7.Kupoteza taarifa muhimu
Ili kujisajili katika mitandao ya kijamii imekua ikidai baadhi ya taarifa ambazo imekua ikiziainisha hivyo watu wengine wasio wema kuweza kuzitumia vibaya.hivyo ni vyema kua makini wakati wa kujisajili katika mitandao ya kijamii ujue kwa nini unajisajili na ujue nini madhara au faida ya tarifa unazojaza hiyo imetokea kwa watu mbalimbali hivyo twapaswa kua makini katika hilo na kuifahamu vizur mitandao hiyo.
Nashauri tuache kuhesabu likes comments responses na kupoteza mda mwingi katika mitandao hii ya kijamii tutumie mda mwingi kujifunza na kuchukua mambo mazuri na kujua kwamba hakuna mafanikio kirahisi kama vile mitandao ya kijamii imekua ikidanganya watu mbalimbali ambao ukikutana nao unasikitisha be you know anything you want in life you have to earn it nothing comes for free trust in God work work.
Personal & Corporate Growth Coach/Author
Stanley Mkolangunzi-Phone:+255 764098564
Comments
Post a Comment